Matokeo Simba vs Yanga Kujulikana Kibarua cha Omog

Matokeo Simba  vs Yanga Kujulikana Kibarua cha Omog
Kufuatia matokeo mabaya waliyopata mabingwa wa kombe la FA Simba SC dhidi ya Mlandege ya visiwani Zanzibar mchezo wa kirafiki uliyopigwa usiku wa jana, mashabiki wa klabu hiyo wamemtaka kocha mkuu mcameroon, Joseph Omog atimuliwe mapema.Simba ambayo imeweka kambi viziwani Zanzibar kwaajili ya kujiwinda na mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya hasimu wake Yanga SC mchezo unaotarajiwa kupigwa Agosti 23 mwaka huu ilikubali kutoka sare tasa ya bila kufungana na Mlandege  jambo ambalo halikutarajiwa na wengi kutokana na usajili waliyoufanya msimu huu hivyo kupelekea wapenzi watimu hiyo kumtolea uvivu kocha huyo.Mashabiki wa timu hiyo wamesikika akisema “Kocha hatumtaki tena hatufai aende zake kwanza hata alivyokuwa Azam yeye ushindi wake ulikuwa mwembamba sare ndiyo nyingi hajui kupanga kikosi, asepe mapema ila ngoja mechi ya Yanga iishe tukitoa sare out, tukifungwa out, tukishinda moja out, hatufai aje Ndailagije muone moto wake,”.


Share on Facebook