Mwanaume Akamtwa Akiwa Amevaa vazi la Kike la Hijab


Jeshi la Polisi mkoani Pwani limemkamata kijana mmoja mkazi wa Mbagala jijini Dar es salaam akiwa amejibadilisha sura kwa kuvaa mavazi ya kike na kujifunika kwa hijabu.

Akizungumzi tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shana amewaambia waandishi wa habari kwamba, kijana huyo amekamatwa eneo la picha ya Ndege barabara ya kwenda Magereza wilayani Kibaha baada kupata taarifa kutoka watu waliomuona na kumtilia shaka nyenendo zake.

Matukio ya wanaume wanaovalia mavazi ya kike na kufunika nyuso zao ili kutekeleza vitendo vya kihalifu yameanza kuongezaka ambapo siku za hivi karibuni Polisi waliwaua watu watatu ambao majina yao hayajatambulika kwa kuwapiga risasi karibu na daraja la Mto Mkapa, wilayani Ruji waakidhaniwa kuwa ni majambazi.

Kamanda wa Polisi alisema watu hao ambao wote ni wanaume walikuwa wameficha nyuso zao kwa hijabu na walikaidi agizo la
polisi kila walipotakiwa kusimama.
Share on Facebook