Yanga kusepa na wachezaji 22

Jumla ya wachezaji 22 na viongozi wa Benchi la Ufundi la Yanga kesho saa 11:30 alfajili wanatarajia kusafiri kwa basi kuelekea Singida kwa ajili ya kupambana na Singida United.
Timu hizo, zinatarajiwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Namfua huko Singida katika mechi ya LigI Kuu Bara.

Yanga inatarajiwa kusafiri bila ya nyota wake muhimu wanne, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko ambao majeruhi na Juma Abdul anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Timu hiyo, ilifanya mazoezi yake ya mwisho saa 3:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi na Singida inayofundishwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Mholanzi, Hans Pluijm.

Katika mazoezi hayo, kocha wa timu hiyo  alionekana akiwapa mbinu mbalimbali za aina ya uchezaji ndani ya uwanja ili kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mechi hiyo.
Share on Facebook