Wema, Idris Watajwa katika Sakata la Kutimuliwa Wasanii Wawili MJ Records

Wakati mjadala ukiendelea baada ya wasanii wawili wa kike, Haitham Kim na Nini kutimuliwa katika label ya MJ Records na producer Daxo Chali, suala hilo limechukua sura mpya mara baada ya Idris Sultan na Wema Sepetu kutajwa.

Taarifa za awali zilieleza kuwa kutimuliwa kwa wasanii wao ni kutokana na mmoja wapo kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Nay wa Mitego kitu ambacho kilidaiwa kinaweza kuchafua brand ya label hiyo.

Hata hivyo Haitham Kim amefunguka mambo mengine kwa kile kilichokuwa kikidaiwa anatoka kimapenzi na Idris kitu kilichopelekea pia kutimuliwa MJ Records. Akizungumza na E-Newz ya EATV Haitham amesema jambo hilo halina ukweli wowote bali ni watu tu wanazusha.

 â€œNi watu tu wametengeneza kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya Haitham na Idris kwa sababu ukiangalia Wema pia ni mtu ambaye hakusapoti hiyo kazi ya Play Boy, so watu wanaendelea kujiuliza kwanini Wema hakusapoti, hivyo sababu inaweza kuwa ni hiyo lakini yule siyo sababu” amesema.

“Mimi nina mpenzi wangu na Idris ana maisha yake, so siwezi kumuingiza Idris kwenye maisha yangu ya mahusiano kwa sababu I have a boy friend, nishamposti hata kwenye social media fans wangu wanamjua” Haitham ameongeza.

Chini ya MJ Records Haitham ameweza kutoa ngoma mbili official, ya kwanza ikiwa ni ‘Fulani’ aliyomshirikisha Mwana FA na Play Boy ambayo sauti ya Wema Sepetu inasikika ndani yake.
Share on Facebook