Tshishimbi apewa tuzo

Vicent Kigosi ‘Ray’ akikabidhi zawadi kwa wachezaji wa Yanga Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba Tshishimbi na kipa Rostand Youthe.

KUNDI kubwa la mashabiki wa Yanga maarufu kama Yanga For Life, jana Jumanne lilitoa zawadi ya fedha na vifaa vya kuchezea mpira kwa wachezaji Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba Tshishimbi na kipa Rostand Youthe.

Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika Makao Makuu ya klabu hiyo yaliy­opo mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Ju­matano, Vicent Kigosi ‘Ray’ ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo alisema Ajibu amezawadiwa shilingi milioni moja baada ya kuchaguliwa mchezaji bora kwenye mechi mfululizo za Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar na Stand united.

Ray ambaye ni msanii wa Bongo Mov­ie nchini alimtaja kiungo Tshishimbi kuwa ameshinda tuzo ya mche­zaji bora wa mechi dhidi ya Simba na kuzawadiwa shilin­gi 500,000, viatu vya mpira ‘njumu’ na vikinga ugoko ‘shine guard’.

Aliongeza kuwa, kipa Mcameroon, Rostand Youthe amepewa shilingi 250, 000 na viatu vya mpira na vi­kinga ugoko kuto­kana na mchango alioutoa tangu aanze kuichezea timu hiyo.
Share on Facebook