Ombi la Singida United lapitishwa

Bodi ya Ligi Tanzania TPLB imetoa kibali rasmi kwa klabu ya soka ya Singida United kuanza kutumia uwanja wake wa Namfua kama uwanja wa nyumbani kwenye mechi zake za ligi kuu msimu huu.

Bodi imeziandikia barua timu zote 16 za ligi kuu kuzifahamisha juu ya Singida United kuhama kutoka uwanja wa Jamhuri Dodoma ambao ilikuwa inautumia kama uwanja wake wa nyumbani na sasa itarejea Singida kwenye uwanja wa Namfua.

Uwanja huo wa Namfua utaanza kutumika Jumamosi hii Novemba 4 kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara raundi ya 9 ambapo Singida United itacheza na mabingwa watetezi Yanga.

Singida United wamewaaga rasmi mashabiki wao wa  mkoani Dodoma na kuwatakia kila la kheri na timu yao ya Dodoma FC wakiwaombea ipande daraja ili mwkaani waweze kushuhudia uhondo wa Ligi Kuu.


Share on Facebook