Ushauri: Kila Nikirudi Nyumbani Nakuta Msichana wa Kazi Anaangalia 'Porn'

Mimi nimeoa na ninaishi na mke wangu lakini hatujabarikiwa kupata mtoto na wote tunafanya kazi mke wangu serikalin na mimi kwenye kampuni moja hapa mjini Dar kutokana na ubize wa kazi tuliamua kutafuta mfanyakazi na hivyo kuletewa huyu mdada wa kazi kutoka kijijini kwao na mke wangu, na mimi na mke wangu hua tunatoka asubui na kurudi jioni hua nampitia kazini tunarudi nyumbani baada ya kazi.

Huyu mdada wa kazi mke wangu alishanieleza kua anatoka kwenye mazingira magumu sana hivyo pamoja na kutufanyia kazi tuwe tunawakumbuka wazazi wake kwa chochote pale tunapojaliwa uwezo na mm nimekua nikifanya hivyo kama msaada kwa wazazi wa huyu binti.

Kilichofanya niombe ushauri kwenu ni kwamba, miezi miwili iliyopita nilisahau document za kazini nyumbani hivyo nilirudi kuzichukua kitu ambacho si kawaida mimi kurudi nyumbani mchana, kitu cha kushangaza nilimkuta huyu binti wa kazi ameweka mkanda wa porn(X) anaangalia na yupo exited aliponiona akashtuka sana na kuniomba msamaha basi mimi nikachukua nilichokua nimesahau na kurudi kazini kwangu huku nikiacha nimemkanya na kuchukua ile CD na kuiharibu.

Sikumwambia mke wangu kwani yeye hua na hasira sana na kwa hali ile angemrudisha huyu mtumishi wetu wa ndani kwao, sikumwambia kwa sababu huyu binti hana msaada wowote na wazazi wake wana hali mbaya huko kijijini nilijua mke wangu akimfukuza ataenda kuteseka sana kwahiyo nikawa na siri moyoni as a man.

Cha kushangaza ni kwamba leo pia nimerudi nyumbani gafla nimemkuta anafanya mchezo ule ule kaweka CD ya X amejiachia kwa sofa amerelax anaangalia hana wasiwasi huyu binti wa miaka 16 aliponiona akapanic na kulia nimsamehe tena nikampa vibao viwili nikachukua kilichonipeleka then nikarudi kazini.

Hapa najiuliza ndugu zangu nimwambie mke wangu kwa maana atamtimua tu, au nimuonee huruma niendelee kumfichia siri kwa mke wangu kwani nikikumbuka wazazi wake na huyu binti wanavyonililia na kuniona tegemeo lao moyo unarudi nyuma.

Sasa hivi niko na mke wangu tunarudi nyumbani huku kichwani najiuliza kama nimwambie kinachoendelea au laa.

Msaada wa ushauri bila matusi nitauzingatia zaidi.

NASHUKURU
Share on Facebook